Mwanamuziki mwenye utata nchini Kenya, Bahati, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kudai kuwa mashabiki wake wanatamani maisha anayoyaishi na mke wake, Diana Marua.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bahati amepakia video akiwa na mkewe Diana wakifurahia mvinyo (wine) huku wakipigana mabusu hadharani licha ya maneno ya watu.
Katika video hiyo mpya, Bahati amesema kuwa alikuwa anasoma maoni ya mashabiki kuhusu ukosoaji wa video yake ya awali, akisisitiza kuwa wengi wanatamani maisha yao ya kifahari na kimahaba.
Kauli yake imejiri saa chache baada ya mwanamuziki huyo kukosolewa vikali mitandaoni kwa kuchapisha video nyingine akiwa amevaa chupi, hatua iliyozua mjadala mkubwa kuhusu mienendo yake ya kisanii na maisha binafsi.