
Mkali wa muziki nchini Bahati ameingia tena katika mijadala kwenye mitandao nchini baada ya kudaiwa kuiba idea ya wimbo wa ‘For You’ wa msanii wa Bongofleva Marioo
Kulingana na ripoti inayosambaa mitandaoni, inadaiwa Bahati ametumia mdundo na ubunifu wa video wa wimbo huo kwenye wimbo wake mpya wa”Je unanifikiria”, hivyo kuibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa muziki nchini ambao walienda mbali zaidi na kuhoji kuwa msanii huyo amekosa ubunifu kwenye muziki wake.
Hata hivyo Bahati hajetoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo yaliyoibuliwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii.