
Staa wa muziki nchini Bahati amewajibu watu wanaotilia shaka vitu vya thamani ambavyo amekuwa akimzawadi mke wake Diana B katika miaka ya hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram bahati amesema kuwa vitu vyote ambavyo amekuwa akimpa mke wake vinatoka kwa mungu ambaye alimtoa kwenye lindi la umaskani katika mitaa ya mabanda ya mathare.
Hitmaker huyo wa ngoma “Adhiambo” ameenda mbali na kuwapa changamoto watu wanaombeza mitandao wawe na imani pamoja na subira katika maisha kwani mungu pekee ndiye ana uwezo wa kubadilisha maisha ya mtu.
Kauli ya Bahati inakuja mara baada ya shabiki mmoja mapema wiki hii kuhoji kuwa wawili hao ni jirani zake lakini hajawahi mwona diana akiendasha magari mawali aina Mercedez ambazo alipatiwa awali ila amekuwa akimwona akiendesha gari aina na vitz.
Siku ya valentines Bahati alimzawadi Diana Marua gari la shillingi million 10 aina ya Land Cruiser TX pamoja na jumba la kifahari lilogharimu shillingi million 27.
Tukio hili lilipelekea mashabiki kwenye mitandao kuhoji kuwa huenda ni kiki wawili hao wanafanya