
Msanii wa Kenya Bahati ameibuka na kuwatolea uvivu wasanii wanaomtukana mkewe, Diana Marua, kupitia akaunti bandia, akisema wanapoteza muda badala ya kuangazia kazi zao.
Kupitia Instagram, Bahati, ameonekana kuguswa na matusi anayopokea Diana, akiwashambulia wanaoendesha chuki hizo kwa kusema kwamba badala ya kutumia nguvu kumshusha Diana, wanapaswa kumuomba ushirikiano wa kimuziki.
Bosi huyo wa EMB Records amesisitiza kuwa mafanikio ya mkewe hayawezi kuzimwa na chuki, akiwataka wapinzani wake kubadilisha mbinu.
Hii inakuja baada ya Diana kuachia wimbo wake mpya “Bibi ya Tajiri” ambao umeibua gumzo mitandaoni na kupata mapokezi makubwa. Video ya wimbo huo tayari imepata zaidi ya views laki nane ndani ya siku tano pekee tangu kuachiwa, hali inayoonesha kupokelewa vizuri na mashabiki licha ya ukosoaji.