
Klabu ya Barcelona imewasilisha rasmi ombi kwa klabu ya Manchester United ili kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza, Marcus Rashford, kwa mkataba wa mkopo unaojumuisha kipengele cha kumnunua moja kwa moja mwishoni mwa msimu.
Taarifa kutoka vyanzo vya karibu na uongozi wa Barcelona zinaeleza kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo anavutiwa na uwezo wa Marcus Rashford na anaamini atakuwa chachu muhimu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo inayojengwa upya.
Ikumbukwe kuwa Rashford alitumia nusu ya msimu wa 2024/2025 kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa, ambako alionyesha mwangaza wa kurejea katika ubora wake wa zamani. Akiwa na Villa, Rashford alicheza jumla ya mechi 17, akifunga mabao 4 na kutoa pasi 6 za mabao (assists), na hivyo kuchangia jumla ya mabao 11.
Hata hivyo, bado haijafahamika kama Manchester United wako tayari kumwachilia mchezaji huyo kwa mkopo mwingine, ikizingatiwa kuwa ni zao la akademia ya klabu hiyo na bado ana nafasi ya kurejea kwenye kiwango cha juu akiwa na umri wa miaka 27.