Entertainment

Barnaba Classic ampa nyota Diamond Platnumz

Barnaba Classic ampa nyota Diamond Platnumz

Mwanamuziki wa Bongofleva Barnaba Classic ameamua kumpa Diamond Platnumz maua yake akiwa hai kwa kushiriki kwa asilimia kubwa sana kwenye kuufanya mwaka 2022 kuwa wenye mafanikio kwake.

Kupitia Instastory yake amemshukuru Bosi huyo wa WCB kwa kuandika ,”Asante sana Mungu akubariki, umetenda pakubwa sana. Mungu akupe njia njema wengi tufaidike na uwepo wako. Unaroho ya kipekee sana”.

Mwaka 2022 Diamond Platnumz alishiriki kwa asilimia kubwa sana kwenye Album ya Barnaba, “Love Sounds Different” ambayo imempa mafanikio makubwa sana ya kimuziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *