Entertainment

BEBE COOL ABADILI MAWAZO DHIDI YA CINDY SANYU, AMUUNGA MKONO KUTWAA UONGOZI WA CHAMA CHA UMA

BEBE COOL ABADILI MAWAZO DHIDI YA CINDY SANYU, AMUUNGA MKONO KUTWAA UONGOZI WA CHAMA CHA UMA

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool ametangaza hadharani kumuunga mkono Cindy Sanyu kwenye azma yake ya kuongoza chama cha wanamuziki nchini humo licha ya kumkosoa kipindi cha nyuma.

Katika mkao na wanahabari Bebe Cool amesema Cindy ndiye anafaaa kuwasimamia wasanii kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kushawishi wadau wa maendeleo pamoja na serikali kutoa pesa za kufadhilia miradi ya muziki lakini pia anazungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha tofauti na mpnzani wake King Saha.

Hitmaker huyo “Gyenvudde” amesema Cindy ni kiongozi dhabiti asiye terereka na changamoto zozote ikizingatiwa kuwa kipindi cha corona alisimama kidete kuwatetea wasanii licha ya viongozi wengi wa wanamuziki nchini Uganda kukimbia majukumu yao.

Kauli ya Bebe Cool imekuja mara baada ya kumkosoa cindy sanyu mwezi mmoja uliopita kwa kudai kuwa msanii huyo ana roho ya kulipiza kisasi lakini pia ana uwezo wa kustahimili ukosoaji kutoka kwa wapinzani kwa kuwa ni mtu mwenye hasira.

Madai hayo ya Bebe Cool yalimuibua Cindy Sanyu na kusema kwamba ataanza mchakato wa kuwaomba msamaha wasanii wote aliowakosea kipindi cha nyuma kama njia moja ya kupata uungwaji kutoka kwa wanamuziki ambao wanapinga azma yake ya kutwaa uongozi wa urais katika chama cha wanamuziki  nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *