
Msanii Eddy Kenzo amekiri kwamba Bebe Cool alimsaidia kuondokana na kesi iliyokuwa ikimuandama kutoka kwa Luba Events.
Katika mahojiano yake hivi karibuni, Kenzo amesema Bebe Cool alimuunganisha na mawakili walioshughulikia kesi yake dhidi ya promota huyo.
“Alinipigia simu na kuniuliza anawezaje kusaidia. Hakutaka kuniona nikiwa kwenye matatizo. Ni rafiki wa kweli,” alisema.
Utakumbuka Luba Events alimburuza mwimbaji huyo wa ‘Tweyagale’ mahakamani Novemba mwaka 2022 baada ya tamasha la ‘Eddy Kenzo’ kufanya vizuri, akimtuhumu kuvunja mkataba wa kuandaa Tamasha hilo. Luba alieleza kuwa alipata hasara ya takriban shillingi millioni 9 ambayo aliwekeza katika tamasha hilo mwaka 2020.
Kenzo alipigwa marufuku kwa muda kutumbuiza jijini Kampala kabla ya marufuku hiyo kuondolewa na mahakama.
Utakumbuka Eddy Kenzo na Bebe Cool walianza kuwa marafiki baada ya Kenzo kuwa karibu na chama cha NRM, mrengo wa kisiasa ambao Bebe Cool anaunga mkono.