Entertainment

Bebe Cool amjibu Gravity Omutujju kuhusu kustaafu muziki

Bebe Cool amjibu Gravity Omutujju kuhusu kustaafu muziki

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amemjibu Gravity Omutujju baada ya rapa huyo kumshauri astaafu muziki kwa kuwa ana umri mkubwa.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Bebe Cool amemtaka rapa huyo kumlipa pesa kama anatamani aache muziki.

Utakumbuka baada ya Gravity kupata mapokezi kwenye show yake miezi kadhaa huko Cricket Oval, Lugogo aliibuka na kuwachana wasanii bebe cool jose chameleone na Bobi wine akiwashauri wageukia masuala ya kilimo na kuachia wasanii kizazi kipya kuendelea na muziki.

Alienda mbali zaidi na kutoa orodha ya wanamuziki bora nchini Uganda na kuwaacha nje wasanii hao watatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *