Entertainment

Bien wa Sauti Sol amjibu Mchekeshaji Eric Omondi kwa kuwaponda wanamuziki wa Kenya

Bien wa Sauti Sol amjibu Mchekeshaji Eric Omondi kwa kuwaponda wanamuziki wa Kenya

Msanii wa Sauti Sol, Bien amemtolea uvivu mchekeshaji Eric Omondi kwa kukosoa wasanii wa kenya kutokana na kuzembea kuachia nyimbo.

Kupitia ukurasa wake wa instagram bien amemtaka Omondi akome kuwashinikiza wasanii wa Kenya waachie muziki mzuri wakati uchekeshaji umemshinda.

Mkali huyo wa ngoma ya “Inauma” amemtaka Omondi kuwekeza nguvu zake kwenye suala la kufufua tasnia ya ucheshi ambayo kwa mujibu wake imepoteza mwelekeo.

Hata hivyo mashabiki wameonekana kumuunga mkono Bien huku wengine wakimtaka msanii huyo akubali ukweli muziki wa kenya umeshuka kwa kuwa wasanii hawatoi nyimbo nzuri ikilinganishwa na wasanii wa mataifa mengi.

Kauli ya Bien imekuja mara baada ya Eric Omondi kushangazwa na hatua ya wasanii wa Kenya kushindwa kuingiza nyimbo nyingi kwenye chati ya muziki ya Apple Music ambayo imetawaliwa na wasanii wa Nigeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *