
Msanii wa Sauti Sol, Bien Aime Baraza ameonekana kuchukizwa na kitendo cha baadhi ya watu kuiombea serikali iweze kufeli kwenye utendaji kazi wake ili wapate maneno ya kuwachamba waliochagua uongozi wa sasa.
Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram hitmaker huyo wa “Inauma” amewashangaa wanaoendeleza tabia hiyo mitandaoni kwa kusema kuwa huo ni ushamba uliopitiliza ikizingatiwa kuwa msimu wa siasa ulikamilika.
Bien ameenda mbali zaidi na kuwataka wanaoeneza propaganda mtandaoni kuacha kadhia hiyo na badala yake wazipambanie familia zao, kwani zama za kuwazia serikali mabaya zimepitwa na wakati.
Bien amekuwa moja kati ya wasanii ambao wamekuwa mstari wa mbele kuzungumzia masuala ya siasa bila uwoga wowote, utakumbuka juzi kati alishinikiza serikali kupunguza bei ya unga wa sima kwa kuwa wakenya wengi wanapitia wakati mgumu kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.