Entertainment

Billie Eilish, Eminem, na Beyoncé Wang’ara Tuzo za American Music Awards 2025

Billie Eilish, Eminem, na Beyoncé Wang’ara Tuzo za American Music Awards 2025

Tuzo za American Music Awards (AMAs) 2025 zimefanyika rasmi mjini Las Vegas usiku wa kuamkia Mei 26, zikishuhudia wasanii wakubwa wakituzwa kwa mafanikio yao ya mwaka. Billie Eilish ndiye aliyeibuka kidedea kwa kushinda tuzo saba, ikiwemo Msanii Bora wa Mwaka, Albamu Bora (Hit Me Hard and Soft), na Wimbo Bora (“Birds of a Feather”).

Miongoni mwa washindi wengine ni Bruno Mars aliyechukua tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa Pop, Beyoncé aliyeshinda kupitia kipengele cha Country, na Eminem aliyeshinda Albamu Bora ya Hip-Hop kupitia kazi yake The Death of Slim Shady. SZA, The Weeknd, Kendrick Lamar, Bad Bunny, na Lady Gaga pia walitambuliwa kwa mchango wao mkubwa katika muziki.

Msanii wa Afrika Kusini Tyla alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Afrobeats, huku RM wa BTS akichukua tuzo ya Msanii Bora wa K-Pop. Janet Jackson alitunukiwa Tuzo ya ICON kwa mchango wake mkubwa katika muziki, naye Rod Stewart alipokea Tuzo ya Mafanikio ya Maisha.

Hafla hiyo ya kifahari ilijumuisha maonyesho ya kuvutia kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Gwen Stefani, Gloria Estefan, na Lainey Wilson, na ilitangazwa moja kwa moja kupitia televisheni ya CBS na huduma ya Paramount+. Mashabiki walifurahia usiku wa muziki uliosheheni burudani na heshima kwa vipaji vikubwa duniani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *