
Angella Katatumba ni moja kati wasanii ambao wamedumu kwenye tasnia muziki nchini uganda kwa muda mrefu.
Licha ya kuanza muziki miaka 15 iliyopita, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 46 amekuwa akipambana kuupeleka muziki wake kimataifa.
Wakati alikutana na prodyuza Daddy Andre mwaka wa 2018 walirekodi wimbo wa pamoja uitwao “Tonelabira” ambao ulikuja ukawa mkubwa sana nchini Uganda mwaka wa 2019.
Hata hivyo walikuja wakakosana vibaya baada ya wawili hao kuchanganya raha ya mapenzi na muziki, jambo lilompelekea Angella katatumba kusuasua kimuziki.
Sasa taarifa mpya mjini ni kwamba lebo ya muziki ya Black Market Records imetoa rai kwa prodyuza Daddy Andre kumshika tena mkono Angella Katatumba kama njia kufufua muziki wake.
Kulingana na chanzo cha karibu na lebo ya Black Market, Daddy Andrea ana mpango wa kumtayarishia Angella Katatumba nyimbo nne kali mwaka huu wa 2022 ambazo zitakuwa moto wa kuotea mbali.
Utakumbuka wawili hao kwa sasa wana wimbo wa pamoja uitwao “Wendi” ambao unafanya vizuri kwenye chati mbali mbali nchini uganda.