
Wimbo wa msanii camila cabello kutoka nchini Cuba uitwao “Havana” uliotoka mwaka wa 2017 ambao amemshirikisha rappa Young Thug, umefanikiwa kuuza (units) millioni 10 ambayo ni ngazi ya juu kabisa.
Camila ambaye ni member wa kundi bora la muziki kuwahi kutoka ulimwenguni la fifty harmony, kutokana na hatua hiyo chama cha Recording Industry Association of America (RIAA) kimekabidhi tuzo maalumu yaani (Plaque) maarufu kwa jina Almasi au (Diamond).
Camila Cabello anakuwa msanii wa kwanza kutoka Cuba kufikia mafanikio hayo makubwa kupitia wimbo mmoja.
Lingine usilo lijua kuhusu “Havana” ni kuwa, rappa Young Thug ambaye ndiye kashirikishwa kwenye wimbo huo, hakutaka kutia verse yake katika havana kutokana na kutoielewa wimbo huo lakini kwa shinikizo la mama yake mzazi alifanya.
Kwenye mahojiano na HipHop DX, Thug ameeleza kwamba hakuamini kama wimbo huo ungefanya vizuri kutokana na kuwa havikua vitu vyake lakini anafurahishwa kuona amekuwa moja ya watu walioshiriki katika wimbo huo ambao umetunukiwa tuzo maalumu ya Diamond na RIAA.