
Msanii Cartoon 47 ameonesha kutoridhishwa na mapokezi ya wimbo wake mpya uitwao Haiwezi ambao amemshirikisha Stevo Simple Boy na Ntosh Ngazi.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Cartoon 47 amesema watu wamekuwa wakimchukulia stevo kama mmiliki wa wimbo huo wakati yeye ndiye aligharamia mchakato wa kutayarisha wimbo wenyewe kwa kumleta Ntosh Gazi kutoka Afrika Kusini.
Aidha ameenda mbali zaidi na kusema kwamba jambo hilo limepelekea baadhi ya mapromota kuanza kumpendelea Stevo kwenye shoo zao huku wakimtenga.
Hata hivyo ametoa wito kwa wadau wa muziki nchini kutomchukulia poa kwenye muziki wake na badala yake watambua pia mchango wake kwenye mafanikio ya wimbo huo.
Wimbo huo uitwao Haiwezi wenye mahadhi ya Amapiano unafanya vizuri kwenye majukwaa mbali mbali ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni ambapo kwenye mtandao wa youtube ina zaidi ya views laki 1 ndani siku 5 tangu iachiwe rasmi.