
Mwanamuziki wa bendi nchini Uganda Catherine Kusasira ameitaka Idara ya polisi nchini humo kumuomba msamaha kwa kusitishwa onesho lake mapema wiki hii bila sababu za msingi.
Katika video aliyochapisha kwenye mitandao yake ya kijamii Kusasira ametoa wito kwa serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria maafisa wakuu wa polisi waliofuta show yake iliyokuwa imewavutia zaidi ya watu 3000 kwenye mkesha wa pasaka.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “I love you” amesema polisi walimvunjia heshima huku akisisitiza kuwa lazima wamuombe radhi kwa kitendo chao cha kusitisha show yake ghafla ikizingatiwa kuwa yeye ni mfuasi mkubwa wa chama cha nrm kilimchompelekea rais Yoweri Museveni kushinda uchaguzi wa mwaka wa 2021.
Utakumbuka baada ya polisi kusimamisha show yake saa tatu usiku wa kuamkia jumatatu kuu ya pasaka mashabiki walighadhabishwa na hatua hiyo ambapo walivunja viti kwenye bustani ya Palms Park Ndejje, Kanaaba huku wengine wakitoweka na viti vingine jambo lilowaacha waandaji wa show hiyo wakikadiria hasara kubwa.