Entertainment

CHAMELEONE NA BOBI WINE WAMALIZA TOFAUTI ZAO

CHAMELEONE NA BOBI WINE WAMALIZA TOFAUTI ZAO

Mastaa wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone na Bobi wine hatimaye wamemaliza ugomvi wao uliodumu kwa kipindi cha miaka miwili.

Hii ni baada ya wawili hao kukutana kwenye hafla ya kusherekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwanamuziki eddy yawe mapema wiki ambapo walipata wasaa mzuri wakuzungumza huku wakionekana wakiwa na nyuso za tabasamu.

Taarifa za Bobi wine na Chameleone kumaliza bifu yao imethibitishwa na Eddy Yawe  ambaye ni kaka wa Bob Wine kwa kusema kwamba amefurahishwa na hatua ya wawili wao kuitikia mwaliko wake huku akisisitiza waendelee kuwa marafiki licha ya utofauti wao wa kisiasa.

Hata hivyo mashabiki wa muziki nchini Uganda wamewapongeza wawili hao kwa hatua ya kumaliza tofauti zao huku  wakiwataka waachie wimbo wa pamoja utakaothibitisha kuwa wamemaliza ugomvi wao.

Utakumbuka  Chameleone aliingia kwenye ugomvi na Bobi Wine mwaka wa 2020 baada ya Bobi Wine kumnyima tiketi ya kuwania kiti cha umeya wa jiji la kampala  kupitia chama cha kisiasa cha NUP.

Tangu wakati huo Chameleone amekuwa akimshambulia Bobi Wine pamoja na watu wake wa karibu kwa hatua ya kuwa kizingiti kwenye azma yake ya kuwa mwanasiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *