
Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca, ameonesha kutoridhishwa na uamuzi wa La Liga wa kuurudisha nyuma mchezo wa Real Betis dhidi ya Valencia, hatua inayowapa wapinzani wao siku mbili zaidi za maandalizi kuelekea fainali ya UEFA Conference League dhidi ya Chelsea, itakayopigwa Mei 28, 2025.
Awali, mechi ya Betis na Valencia ilikuwa imepangwa Jumapili ya Mei 25, lakini sasa itachezwa Ijumaa ya Mei 23, ili kuipa nafasi Betis kupumzika. Huku Chelsea wakilazimika kusafiri kuikabili Nottingham Forest katika mechi ya mwisho ya EPL inayotajwa kuwa ya kuamua hatma yao ya kufuzu kwa UEFA Champions League 2025/26.
Maresca amesema hali hiyo ni ya kutokuwa na usawa wa kimashindano, akisisitiza kuwa maandalizi yao kwa fainali hiyo sasa yatakuwa na changamoto zaidi.
Fainali hiyo inatarajiwa kuchezwa mjini Athens, Ugiriki, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona iwapo Chelsea watachukua taji hilo au kama Real Betis watachukua faida ya muda wa ziada wa maandalizi.