Entertainment

Chris Brown Aachiliwa kwa Dhamana ya Dola Milioni 6.7 London

Chris Brown Aachiliwa kwa Dhamana ya Dola Milioni 6.7 London

Msanii mashuhuri wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown, ameachiwa kwa dhamana ya dola milioni 6.7 (takriban Shilingi bilioni 1) na mahakama mjini London baada ya kufunguliwa mashtaka ya kushambulia mtu bila sababu katika kilabu usiku mnamo mwaka 2023.

Chris Brown mwenye umri wa miaka 36, ambaye ameshawahi kushinda tuzo ya Grammy, bado hajaombwa kutoa ombi la kukiri au kukataa shtaka hilo. Hata hivyo, masharti ya dhamana yake yanamruhusu kuanza ziara yake ya kimataifa mwezi ujao kama ilivyopangwa awali.

Msanii huyo alikamatwa wiki iliyopita na baadaye kushtakiwa kwa kosa la kujeruhi kwa makusudi, kufuatia tukio ambalo inadaiwa alimshambulia mtayarishaji wa muziki kwa chupa ya kileo aina ya tequila.

Jaji Tony Baumgartner alisema kuwa Brown anaruhusiwa kuendelea na ziara yake, ikijumuisha maonesho kadhaa nchini Uingereza, lakini lazima alipe dhamana hiyo ili kuhakikisha atahudhuria kesi yake mahakamani.

Tukio hilo limezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wanamuziki wenzake, huku wengi wakisubiri kwa hamu kuona hatima ya kesi hiyo inayomkabili mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *