Entertainment

Chris Brown Ashikiliwa Rumande Hadi Juni 13 kwa Tuhuma za Kujaribu Kumdhuru Mtayarishaji wa Muziki

Chris Brown Ashikiliwa Rumande Hadi Juni 13 kwa Tuhuma za Kujaribu Kumdhuru Mtayarishaji wa Muziki

Msanii maarufu wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown, ataendelea kushikiliwa rumande hadi tarehe 13 Juni 2025, akisubiri kufikishwa tena mahakamani kufuatia tuhuma za kushambulia kwa makusudi.

Chris Brown anadaiwa kumshambulia mtayarishaji wa muziki Abraham Diaw kwa kutumia chupa katika kilabu cha usiku jijini London mnamo Februari 2023.Tuhuma hizo zinahusiana na kosa la kusababisha madhara makubwa ya mwili kwa nia ovu (grievous bodily harm with intent), ambalo ni miongoni mwa makosa makubwa kisheria nchini Uingereza.

Hadi sasa, Brezzy hajatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo, huku wakili wake akisisitiza kuwa msanii huyo ataendelea kushirikiana na vyombo vya sheria hadi ukweli utakapobainika.

Mashabiki na wadau wa muziki duniani kote wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya kesi hii, ambayo huenda ikaathiri ratiba na kazi za kisanii za Brown kwa kiasi kikubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *