Entertainment

CINDY SANYU AMKINGIA KIFUA EDDY YAWE KWA TUHUMA ZA KINGONO

CINDY SANYU AMKINGIA KIFUA EDDY YAWE KWA TUHUMA ZA KINGONO

Rais wa chama cha wasanii nchini Uganda Cindy Sanyu amedai kuwa hana uwezo wa kumsaidia msanii chipukizi Sumaiya Sheebah ambaye alidai kuwa alinyanyaswa kijinsia na Eddy Yawe.

Cindy amesema mrembo huyo ana ushahidi wowote wa kuonyesha alidhulumiwa kingono na Eddy Yawe kwa kuwa hana mkataba wa kufanya kazi na msanii, hivyo itakuwa vigumu kumsaidia kisheria.

Hitmaker huyo wa “Local Man” ametoa changamoto kwa wasanii kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya kufanya kazi na wasanii wenzao kama njia ya kuwasaidia kisheria wakati wa matatizo.

Utakumbuka juzi kati msanii chipukizi Sumaiya Sheebah aliibua madai kuwa Eddy Yawe amekuwa akimuitisha rushwa ya ngono ili waweze kufanya kazi ya pamoja, shutuma ambazo bosi huyo wa Dream Studios alikanusha vikali kwa kusema kwamba madai ya mrembo huyo hayana ukweli wowote kwani ni njia ya kuichafua brand yake ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *