Entertainment

Content Creators Wa Kenya Wamuacha Chief Godlove na Hasara

Content Creators Wa Kenya Wamuacha Chief Godlove na Hasara

Billionea Chief Godlove anakadiria kupata hasara ya maelfu ya pesa baada ya gari lake kupasuliwa kioo ndani ya Nairobi CBD, tukio lililotokea wakati akikutana na content creators mbalimbali jijini humo.

Licha ya hasara hiyo, Chief Godlove amesema tukio hilo liligeuka kuwa ushuhuda wa upendo mkubwa na mshikamano wa dhati kutoka kwa content creators wa Kenya. Ameeleza kuwa alichokutana nacho siku hiyo kilizidi thamani ya hasara aliyopata, kwani alipokea faraja, moyo wa kujali na sapoti kubwa kutoka kwa watu aliokutana nao.

Kwa mujibu wake, ingawa kioo cha gari lake kilipasuka katika hali ya msongamano na juhudi za watu kulazimisha kumuona, tukio hilo lilimfunulia ukubwa wa upendo aliokuwa nao kutoka kwa jamii ya waandaaji wa maudhui.

Kutokana na kuguswa na tukio hilo, Chief Godlove ametangaza kuwa Jumapili ijayo content creators wote watakutana Nairobi CBD, ambapo ameahidi kugharamia chakula na vinywaji vyote kama ishara ya shukrani kwa upendo alioupokea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *