Msanii wa muziki kutoka Kenya, Bahati, amewashangaza mashabiki wake baada ya kuwaomba hadharani wamsaidie kwa kumpa ushauri wa mambo anayopaswa kubadilisha au kuboresha kuelekea mwaka wa 2026.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Bahati amesema kuwa mwaka mpya unampa nafasi ya kujipima upya kama msanii, mume na baba, huku akisisitiza kuwa maoni ya mashabiki wake yana mchango mkubwa katika safari yake.
Msanii huyo, amesema kuwa yuko tayari kusikiliza ukosoaji wa kujenga, iwe ni kuhusu muziki wake, tabia, mawasiliano na mashabiki, au mwelekeo wa maisha kwa ujumla.
Bahati amesema atayapitia maoni yote na kuyazingatia kwa makini, akisisitiza kuwa yuko tayari kubadilika pale inapobidi kwa ajili ya familia yake, mashabiki na mustakabali wake kama msanii.