Gossip

D Voice Aapa Kulinda Heshima ya Mama Yake Mitandaoni

D Voice Aapa Kulinda Heshima ya Mama Yake Mitandaoni

Msanii wa muziki wa Singeli, D Voice, ameapa kupambana vikali na yeyote atakayemdharau au kumtusi mama yake mzazi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kushuhudiwa ongezeko kubwa la mashabiki wanaowatusi wasanii kwa matusi makali yanayohusisha wazazi wao.

Akizungumza kwenye mahojiano yake hivi karibuni, D Voice amesema hatavumilia kuona mzazi wake akivutwa kwenye migogoro ya mitandaoni, akisisitiza kuwa atakayemtukana mama yake, naye atamlipiza kwa kumtukana mama yake pia.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Baby Mpya, amesema ana hazina kubwa ya matusi yenye misamiati ya uswahilini ambayo wengi hawaifahamu, akionya kuwa mtu yeyote atakayeanza matusi kwa bi mkubwa wake anajitakia matatizo.

D Voice, amesisitiza kuwa anathamini sana heshima, akisema ni heri mtu amzidi kwa mali au fedha kuliko kumkosea heshima kwa kumtusi mzazi wake. Kwa mujibu wake, heshima kwa wazazi ni jambo la msingi ambalo halipaswi kuchezewa hata kidogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *