D Voice Aapa Kulinda Heshima ya Mama Yake Mitandaoni

D Voice Aapa Kulinda Heshima ya Mama Yake Mitandaoni

Msanii wa muziki wa Singeli, D Voice, ameapa kupambana vikali na yeyote atakayemdharau au kumtusi mama yake mzazi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kushuhudiwa ongezeko kubwa la mashabiki wanaowatusi wasanii kwa matusi makali yanayohusisha wazazi wao. Akizungumza kwenye mahojiano yake hivi karibuni, D Voice amesema hatavumilia kuona mzazi wake akivutwa kwenye migogoro ya mitandaoni, akisisitiza kuwa atakayemtukana mama yake, naye atamlipiza kwa kumtukana mama yake pia. Hitmaker huyo wa ngoma ya Baby Mpya, amesema ana hazina kubwa ya matusi yenye misamiati ya uswahilini ambayo wengi hawaifahamu, akionya kuwa mtu yeyote atakayeanza matusi kwa bi mkubwa wake anajitakia matatizo. D Voice, amesisitiza kuwa anathamini sana heshima, akisema ni heri mtu amzidi kwa mali au fedha kuliko kumkosea heshima kwa kumtusi mzazi wake. Kwa mujibu wake, heshima kwa wazazi ni jambo la msingi ambalo halipaswi kuchezewa hata kidogo.

Read More
 Meja Kunta Atoa Msamaha kwa Jux na D Voice Baada ya Utata wa Wimbo

Meja Kunta Atoa Msamaha kwa Jux na D Voice Baada ya Utata wa Wimbo

Baada ya drama ya muda mitandaoni kuhusu umiliki wa wimbo “Ex Wa Nani”, msanii wa singeli Meja Kunta amevunja ukimya na kutoa maoni yake juu ya sakata hilo, ambalo limewahusisha wasanii Jux na D Voice. Akizungumza na Podcast ya Simulizi na Sauti, Meja Kunta alieleza kuwa hana muda wa kubishana na watu anaowaita “watoto wadogo,” akionyesha msimamo wake wa kutotaka kuendeleza mzozo huo. “Mimi ni mkubwa, sikutaka kubishana na watoto wadogo. Sitaki kupigizana kelele. D Voice anajua mwenyewe alichokifanya na tumeshaongea jana,” alisema Meja Kunta kwa utulivu. Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Jux kuposti kipande cha wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii, hatua iliyozua maswali kutoka kwa mashabiki kuhusu uhalali wa wimbo huo, ambao awali ulitajwa kuwa ni mali ya Meja Kunta. Taarifa zinaeleza kuwa D Voice alimpa Jux wimbo huo bila ridhaa ya Meja, hali iliyochochea mvutano wa maneno. Hata hivyo, Meja Kunta ameonesha ukomavu kwa kufichua kuwa Jux na D Voice walimpigia simu kumuomba msamaha, jambo ambalo linaashiria kutamatika kwa mgogoro huo. Kwa sasa, mashabiki wanasubiri kuona hatma ya wimbo huo na iwapo utafanyiwa marekebisho ya umiliki au utaachiwa rasmi na mmoja wa wahusika waliotajwa.

Read More