Entertainment

Rose Muhando Asema Mungu Alimkataza Kufanya Kolabo na Rayvanny

Rose Muhando Asema Mungu Alimkataza Kufanya Kolabo na Rayvanny

Msanii mkongwe wa muziki wa Injili, Rose Muhando, amefunguka sababu iliyomfanya kukataa kushirikiana na msanii wa Bongo Fleva Rayvanny kwenye wimbo uitwao Ni Mungu unaopatikana kwenye albamu yake The Big One ya mwaka 2024.

Akizungumza na Planet Bongo, Rose Muhando amesema uamuzi wake haukutokana na chuki wala kubeza kipaji cha Rayvanny, bali ni mwongozo wa kiroho alioupata. Kwa mujibu wa msanii huyo, alifanya maombi na kusikiliza sauti ya Mungu kabla ya kufanya uamuzi, ndipo akaelezwa wazi kuwa asifanye wimbo huo.

Muhando ambaye anafanya poa na wimbo wake Mbingu za Mbingu, amebainisha kuwa kila hatua anayochukua katika muziki wake huongozwa na imani na maombi, akisisitiza kuwa analinda wito wake wa muziki wa Injili.

Hata hivyo, Rose Muhando amesisitiza kuwa yupo tayari kushirikiana na msanii yeyote pale tu atakapopata kibali cha Mungu, akisema anataka kazi zake ziendelee kuwa na ujumbe na baraka kwa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *