
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Daddy Owen ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
Album hiyo inayokwenda kwa jina la Chapter 4 ina jumla ya singo 15 ya moto huku ikiwa na 6 collabo pekee.
Daddy Owen amewashirikisha wasanii kama Nakaaya,Bella Kombo, Judy Stevens,Ivyln Mutua,Danco na Slejj.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chapter 4 album Daddy Owen amesema safari ya kuandaa album yake mpya haikuwa rahisi ila anamshukuru mwenyezi mungu kwa kumwezesha kuikamilisha album hiyo licha ya changamoto alizokutana nazo.
Chapter 4 ni album ya sita kwa mtu mzima Daddy Owen lakini pia inavunja ukimya wake wa miaka 5 tangu alipoachia album yake ya Vanity iliyotoka mwaka wa 2016.