Entertainment

Daddy Owen Awataka Wasanii Kuwajibika Baada ya Diamond Kufuta Picha za Kisiasa

Daddy Owen Awataka Wasanii Kuwajibika Baada ya Diamond Kufuta Picha za Kisiasa

Msanii wa muziki wa injili nchini Kenya, Daddy Owen, ametoa wito kwa wasanii barani Afrika kuwa na uwajibikaji mkubwa katika misimamo yao ya kijamii na kisiasa, akisisitiza umuhimu wa kusimama na wananchi badala ya mifumo ya kisiasa.

Kupitia Instagram, Daddy Owen amesema kuwa tukio la Diamond kufuta machapisho ya kisiasa ni funzo kwa wasanii na watu mashuhuri kutambua kuwa sauti zao zina ushawishi mkubwa kwa jamii, hivyo ni muhimu kuzingatia misimamo yenye heshima na inayowakilisha ukweli wa wananchi.

Ameongeza kuwa wasanii hawapaswi kutumia majukwaa yao kuunga mkono mamlaka bila kusikiliza hisia na matakwa ya mashabiki wao. Kwa mujibu wa Daddy Owen, jukumu la msanii ni kuleta matumaini, amani na mshikamano, si kugawanya jamii kupitia misimamo ya kisiasa.

Kauli hiyo imekuja kufuatia hatua ya msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz, kufuta picha na video zote alizokuwa ameweka mtandaoni akimuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, baada ya wananchi nchini humo kupinga matokeo ya uchaguzi uliomalizika juzi na kuzua maandamano makubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *