Entertainment

DAKTARI KWENYE KESI YA TORY LANEZ ATHIBITISHA MEGAN THEE STALLION KUKATWAA NA VIOO

DAKTARI KWENYE KESI YA TORY LANEZ ATHIBITISHA MEGAN THEE STALLION KUKATWAA NA VIOO

Daktari amethibitisha kwamba Megan Thee Stallion hakupigwa risasi mguuni kama anavyodai bali alikatwa na vioo kwenye tukio ambalo linamtaja Tory Lanez kumpiga risasi.

Uchunguzi umebainisha kwamba baada ya kutokea vurugu baina ya washkaji ambao walikuwa pamoja nao kwenye gari, zilipigwa risasi kadhaa ambazo zilivunja vioo vya gari na wakati Megan Thee Stallion akijitahidi kutoka nje ya gari, alivikanyaga na kumuumiza.

Aprili 6 mwaka huu Tory Lanez aliachiwa kwa dhamana ya shilling milllioni 40 za Kenya baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka amri ya mahakama iliyotolewa kumkinga Megan Thee stallion kwenye shtaka lao linaloendelea.

Ikumbukwe Tory Lanez anakabiliwa na Mashtaka mawili ambayo ni kumshambulia rapa Megan thee Stallion mwaka 2020 na pia kubeba silaha yenye risasi kinyume na sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *