
Staa wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ametoa ushauri mzito kwa vijana ambao bado hawajaoa, akiwataka kuacha kudharau miili yao na kupoteza fedha kwa kuwa na wanawake wengi.
Kupitia ujumbe aliouandika SnapChat, Diamond amewaonya vijana kwamba tabia ya kubadilisha wapenzi mara kwa mara haiwezi kuwasaidia kufanikisha ndoto zao wala kuwapeleka popote kimaisha.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa hekima ya kweli ni kujitambua na kuamua kutulia na mpenzi mmoja, au wawili, huku akieleza kuwa kiwango cha juu kabisa kisipite watatu. Aidha, ameongeza kuwa katika hali ya changamoto kubwa, vijana wanaweza kuwa na wanne pekee.
Ushauri huo umewavutia mashabiki wengi mitandaoni, huku baadhi wakipongeza msimamo wa Diamond kama njia ya kuhamasisha vijana kuheshimu maisha yao na kutumia rasilimali zao kwa uangalifu.