
Baada ya kimya cha muda mrefu na stori za hapa na pale kuhusu uwepo wake ndani ya record label ya WcB , hatimae boss wa label hiyo Diamond Platnumz ameamua kuweka wazi juu ya ujio mpya wa first lady wa WCB Queen Darleen
Kupitia insta story yake Diamond Platnumz ameshare sehemu ya video clip ikimuonesha Queen Darleen akiwa studio tayari kwa ajili ya maandalizi ya kazi mpya.
Hitmaker huyo wa “Bachelor” ndiye msanii wa kwanza kwa kike kusainiwa na lebo ya WCB kisha baada ya miaka kadhaa ndipo akaja Zuchu.
Utakumbuka hadi sasa Queen Darleen ndiye msanii pekee ambaye hajatoa albamu wala EP chini ya WCB Wasafi.