Mwanamitandao aliyegeukia muziki Diana B amemkosoa hadharani mume wake, Bahati, kufuatia kuachia video ya wimbo wenye utata uitwao “Seti.”
Diana amemtaka Bahati kuondoa video hiyo ya wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii, akieleza kuwa maudhui yake hayaendani na maadili ya kifamilia. Amesema kuwa hatakuwa tayari kuendeleza uhusiano wao wa kifamilia hadi pale Bahati atakapochukua hatua hiyo, akimhimiza pia kuwa makini zaidi na maisha badala ya kuendeleza mizozo isiyo ya lazima.
Kwa mujibu wa Diana, wasanii wanapaswa kuheshimu taasisi ya ndoa na kuzingatia maadili wanapotayarisha kazi zao za sanaa, kwani jamii huwatazama kama mfano wa kuigwa.
Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa timu ya YouTube haijaona tatizo lolote katika wimbo huo “Seti,” ambao umeendelea kutazamwa kwa wingi na kuvutia maoni mengi kutoka kwa mashabiki wa muziki wa Bahati.