Entertainment

Diana B anyosha maelezo kuhusu video iliyosambaa mtandaoni akikiri kutoka kimapenzi na wanaume wengi

Diana B anyosha maelezo kuhusu video iliyosambaa mtandaoni akikiri kutoka kimapenzi na wanaume wengi

Msaniii na  mwanamitandao maarufu kutoka Kenya Diana Marua amefunguka juu ya video iliyosambaa mtandaoni akikiri kuwa alitembea na wanaume wengi kimapenzi kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya msingi.

Kupitia ujumbe mrefu aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Diana amesema aliweka wazi suala hilo kwa umma kwa lengo la kuwapa moyo vijana wanaopitia masha magumu.

Lakini pia amewahimiza watoto wa kike kutokata tamaa kwenye ndoto zao na badala yake watie bidii kwani muda wao wa kupata mafanikio utafiki.

Diana Marua ameongeza kuwa kama balozi mwema katika jamii anapaswa kuzungumzia magumu aliyoyapitia kwenye maisha yake badala ya kuangazia mazuri tu.

Diana alichapisha video hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii  mwaka 2020 wakati alipokuwa akipokea gari jipya aina Mercedes Benz alilozawadi na mume wake Bahati.

Alikumbuka kipindi alikuwa anaishi maisha ya uchochole ambapo alilazimika kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kwa ajili ya kupata pesa lakini pia kuendesha magari ambayo hakuwa anaweza kumudu wakati huo.

Kwa sasa Diana ana hesabu baraka zake kama Mama ya watoto watano, Mke na mtengeneza maudhui kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *