
Couple pendwa nchini inayoundwa na wasanii Diana B pamoja na Bahati imetangaza jinsia ya mtoto wao wa tatu ambaye atazaliwa hivi karibuni.
Katika hafla ya kutambulisha jinsia ya mtoto huyo wawili hao wameweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kiumemuda wowote kuanzia sasa
Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali wamewapongeza wawili hao kwa hatua hiyo wakati huu wapo mbioni mkaribisha mtoto wao wa watatu.
Utakumbuka juzi kati taarifa zilisambaa mtandaoni kwamba huenda Diana B amejifungua kwa siri kutokana na jumbe zenye ukakasi alizokuwa anachapisha kwenye mtandao wake wa Instagram.