LifeStyle

Diana Bahati Aonyesha Utajiri wake Wakati Mumewe Akikumbwa na Kashfa

Diana Bahati Aonyesha Utajiri wake Wakati Mumewe Akikumbwa na Kashfa

Mke wa msanii Bahati, Diana Marua maarufu kama Diana B, amewajibu kimkakati wanaozidi kumbeza mume wake Bahati ambaye anahusishwa na kashfa ya kushindwa kutimiza ahadi yake ya kutoa KSh1 milioni kwa timu ya taifa, Harambee Stars.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana alionekana akijivunia shopping ya mwezi mmoja iliyogharimu takribani KSh160,000. Bidhaa alizonunua zilijumuisha vyakula, bidhaa za nyumbani na mahitaji mengine ya familia yake.

Hata hivyo, kilichowashangaza wengi ni pale alipoweka wazi wingi wa pesa taslimu alizokuwa nazo nyumbani. Diana alionekana akishika mirundo ya noti za KSh1,000, ambazo alidai zinafikia jumla ya KSh2 milioni.

Wakati mashabiki wengine wakivutiwa na maisha ya kifahari anayoyaonesha, wengi walishangaa hatua yake ya kuonyesha kiasi kikubwa cha fedha hadharani, hasa ikizingatiwa kwamba Bahati anatupiwa lawama kwa kukosa kutimiza ahadi yake ya kifedha kwa wachezaji wa Harambee Stars baada ya ushindi wao mkubwa kwenye mashindano ya CHAN 2024.

Mashabiki mtandaoni wamehoji uhalisia wa pesa hizo, wengine wakisema huenda ilikuwa njia ya Diana kutafuta kiki na kutetea hadhi ya kifamilia wakati jina la Bahati linatikiswa na shinikizo la mashabiki na wanamichezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *