Msanii mkongwe wa muziki wa Kenya, DNA, amefunguka na kueleza sababu zinazowafanya mapromota wengi nchini humo kukataa kumpa nafasi ya kutumbuiza kwenye matamasha ya muziki.
Akizungumza kwa uwazi, DNA amesema moja ya changamoto kubwa inayomkabili ni tabia yake ya kutojipendekeza au kuwabembeleza watu ili apate kazi. Kwa mujibu wake, hali hiyo imefanya baadhi ya mapromota kumweka kando licha ya uzoefu na uwezo wake mkubwa jukwaani.
Msanii huyo pia amedai kuwa mtu aliyewahi kuingia naye kwenye bifu alimfungia milango mingi ya kazi, akisema mhusika huyo anajuana na watu wengi wenye ushawishi ndani ya tasnia ya muziki, jambo lililoathiri nafasi zake za kupata shows.
Akizungumzia uwezo wake wa kutumbuiza, mkali huyo wa ngoma ya “Banjuka” amesema baadhi ya wadau wanaogopa kumpa shows kwa hofu kuwa atawafunika wasanii wengi kwenye suala la performance jukwaani.
Kauli ya DNA imekuja baada ya kujitokeza hadharani na kuwaomba mapromota wampe nafasi ya kazi ya kutumbuiza kwenye shows za kufunga mwaka, akieleza kuwa hali ya kiuchumi imekuwa ngumu.