
Wanamuziki Drake na The Weeknd wameendelea kuziwekea mgomo Tuzo za Grammy, taarifa mpya zinasema wakali hao kutoka nchini Canada hawajawasilisha nyimbo zao kwa ajili ya kufikiriwa (Consideration) kwa tuzo za mwaka 2023.
Album zao ‘Honestly, Nevermind’ na ‘Dawn FM’ hazijawasilishwa kwenye kipengele chochote cha tuzo hizo kwa mwaka 2023 sambamba na nyimbo zao Hit kama ‘Sticky’ na ‘Out Of Time.’
Kwa upande wa Drizzy, amekuwa kwenye mahusiano mabaya na Waandaaji wa tuzo hizo tangu mwaka 2017 baada ya kutoridhika na kipengele ambacho wimbo wake “Hotline Bling” iliwekwa.
Mwaka Jana alitangaza kujitoa kwenye Tuzo hizo baada ya kutajwa kwenye vipengele viwili ambapo alitajwa kuwania Best Rap Album na Best Rap Performance.
Si hayo tu, Drake pia alisimimama kumtetea The Weeknd ambaye mwaka Jana alikosekana kwenye kipengele chochote cha Tuzo za Grammy licha ya kuachia Album “After Hours” ambayo ilifanya vizuri sana.