Gossip

Dudu Baya Amwaibisha Mwijaku kwa Tuhuma Nzito

Dudu Baya Amwaibisha Mwijaku kwa Tuhuma Nzito

Msanii mkongwe wa Bongofleva, Dudu Baya, amemwaibisha hadharani mtangazaji na mdau wa burudani Mwijaku kwa kuibua madai mazito dhidi yake.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Dudu Baya amedai kuwa Mwijaku kwa sasa hana makazi ya kudumu baada ya kudaiwa kufurushwa na mke wake kutoka katika nyumba aliyokuwa akiishi, hatua aliyodai ilitokea baada ya ndoa yao kuvunjika.

Katika madai mengine mazito, Dudu Baya amedai kuwa kipindi Mwijaku alipokuwa akisoma chuoni aliwahi kuhusishwa na sakata la ushoga, kauli ambayo imezua mjadala mpana mitandaoni.

Dudu Baya amejigamba kuwa hana sababu ya kuhangaika na makazi kwani anamiliki majumba mawili ya kifahari. Ameongeza kuwa hata kama mwanamke wake atamuacha, bado hawezi kukosa pa kuishi.

Kauli hizi zimekuja siku chache baada ya Mwijaku kudai kuwa Dudu Baya anaishi kwenye lindi la umaskini kutokana na msanii huyo kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *