Gossip

Whozu Akanusha Kutoka Kimapenzi na Lulu Diva

Whozu Akanusha Kutoka Kimapenzi na Lulu Diva

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Whozu, amekanusha vikali madai yanayotembea mtandaoni zikimuhusisha kutoka kimapenzi na Lulu Diva, rafiki wa mwanamke wake Wema Sepetu.

Kwenye mkao na waandishi wa habari, Whozu amesema madai hayo hayana ukweli wowote, akisisitiza kuwa yeye na chimama wake Wema Sepetu wako vizuri na wanaendeleza upendo wao bila ugomvi wowote.

Msanii huyo, amefafanua hajawahi kuwa chanzo cha mvutano uliopo kati ya Lulu Diva na Wema Sepetu, akibainisha kuwa hataki kuingilia ugomvi wao wala kuwa chanzo cha sintofahamu iliyojitokeza. Amesema anajitahidi kulinda mahusiano yake na Wema Sepetu, hivyo hawezi kujihusisha na mambo yanayoweza kuleta tafrani.

Kauli ya Whozu imekuja kufuatia madai yaliyoibuliwa na Juma Lokole, aliyedai kuwa Whozu na Lulu Diva wamekuwa wakitoka kimapenzi kwa muda. Madai hayo yalidaiwa kuwa chanzo cha Wema Sepetu kukasirika na kukataa kuendelea na mahusiano, akihisi kusalitiwa na watu aliokuwa anawaamini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *