Gossip

Dulla Makabilla Awataka Wasanii Wasijilinganishe Naye Kwa Utajiri

Dulla Makabilla Awataka Wasanii Wasijilinganishe Naye Kwa Utajiri

Msanii wa Singeli, Dulla Makabilla, amewataka wasanii nchini Tanzania kuacha kujilinganisha naye kwenye masuala ya fedha, akisema kwa sasa amejitawaza rasmi kuwa tajiri na hana mpango wa kushindana na mtu kwenye kipato.

Kwenye Mahojiano na Bongo 5, Makabilla amesema wasanii wanaopenda mashindano ya mali au kuonyesha utajiri hawapaswi kumchukulia kama kipimo cha mafanikio hayo.

Msanii huyo, amefafanua kuwa eneo pekee analoona linafaa kwa ushindani ni kwenye muziki, ambako anataka kuona ubunifu, ubora wa kazi, na uwezo wa kutoa nyimbo zinazowafikia mashabiki.

Kwa kauli yake, Makabilla anasisitiza kuwa mafanikio ya kweli yanapimwa kwa ubunifu na mchango wa muziki, na si kwa mali au utajiri unaoonyeshwa hadharani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *