LifeStyle

Khaligraph Jones Afunguka Sababu za Kwenda Gym Kila Siku

Khaligraph Jones Afunguka Sababu za Kwenda Gym Kila Siku

Rapa Khaligraph Jones amefunguka sababu inayomsukuma kuendelea na utaratibu wa kufanya mazoezi ya gym kila siku.

Kupitia Instastory yake, Khaligraph amesema kuwa hofu ya kukosolewa mitandaoni endapo angeonekana kunenepa kupita kiasi ndiyo sababu kuu ya nidhamu yake ya mazoezi.

Khaligraph anaamini kuwa mashabiki na wakosoaji mitandaoni mara nyingi hawana huruma na huwa wakali wanapotoa maoni kuhusu muonekano wa wasanii.

Rapa huyo amesema hali hiyo imemfanya kujitolea kuhakikisha anabaki katika hali bora ya kiafya na kimwili, ili kuepuka maneno ya kejeli na ukosoaji wa umma.

Mashabiki wake wamechukulia kauli hiyo kwa mitazamo tofauti, wengine wakiipongeza kama dalili ya uwazi na kujituma, huku wengine wakisema kuwa wasanii wengi wanaishi chini ya shinikizo la kuhifadhi mwonekano fulani ili kuepuka ukosoaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *