Entertainment

Eddy Kenzo Afunguka Sababu ya Kukataa Mikataba Kubwa ya Muziki

Eddy Kenzo Afunguka Sababu ya Kukataa Mikataba Kubwa ya Muziki

Mwanamuziki nyota kutoka Uganda, Eddy Kenzo, amefunguka kuhusu sababu za kukataa kusaini mikataba na kampuni kubwa za muziki duniani, zikiwemo Sony Music na Universal Music Group.

Kenzo, ambaye ni miongoni mwa wasanii waliotukuka zaidi nchini Uganda na mwenye tuzo kama BET Award pamoja na uteuzi kadhaa wa Grammy, amesema amepewa ofa nyingi lakini amezikataa kwa makusudi licha ya mafanikio yake ya kimataifa.

Akipiga stori na kituo kimoja cha habari, Kenzo amesema lebo kubwa mara nyingi huwabana wasanii kama gereza, na kuwanyima uhuru wa kufanya maamuzi ya kibunifu. Anadai kuwa kampuni hizo hutanguliza maslahi ya kibiashara kuliko ustawi wa msanii.

Kenzo pia ametaja kuwa ameshuhudia mifano ya wasanii waliopitia wakati mgumu chini ya mikataba ya muda mrefu na lebo kubwa, akisema wengine hupoteza mwelekeo au kupungua kwa ubunifu.

Hitmaker huyo wa Nsimbudde, anasisitiza kuwa kujitegemea kumempa nafasi ya kujiamulia mambo muhimu bila shinikizo, na kumwezesha kuendelea kujijenga kimataifa kwa njia anayoiona bora kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *