Entertainment

Eddy Kenzo Amshutumu Bebe Cool Kwa Roho Mbaya na Njama Dhidi ya Wasanii

Eddy Kenzo Amshutumu Bebe Cool Kwa Roho Mbaya na Njama Dhidi ya Wasanii

Msanii nyota kutoka Uganda, Eddy Kenzo, amemshutumu Bebe Cool kwa madai ya kuwa na roho mbaya dhidi ya wasanii wengine na kutumia ushawishi wa kisiasa kujinufaisha binafsi huku akiwadhoofisha wenzake.

Kwa mujibu wa Kenzo, Bebe Cool amekuwa akijipendekeza kwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kwa lengo la kupata nguvu na nafasi ya kuwazima wasanii wengine ndani ya tasnia ya muziki. Kenzo anadai kuwa ushirikiano huo wa karibu na serikali umekuwa ukitumika kama chombo cha kudhibiti na kunyamazisha sauti za wasanii wasiokubaliana na msimamo wa Bebe Cool.

Kenzo anadai Bebe Cool alijaribu kukimbia na fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kusaidia wasanii, hali iliyoibua mgogoro mkubwa kati yao. Kenzo anasema fedha hizo zilipaswa kuwafikia wasanii wengi, lakini kulikuwa na njama za kuzimiliki kinyume na makubaliano.

Ikumbukwe kuwa Eddy Kenzo na Bebe Cool wamekuwa kwenye timu moja ya kampeni ya Rais Yoweri Museveni, wakishiriki katika shughuli mbalimbali za kuhamasisha vijana na wasanii kumuunga mkono kiongozi huyo. Hata hivyo, inadaiwa kuwa uhusiano wao ulianza kuyumba baada ya fedha zilizotolewa na serikali kwa wasanii kuibua mvutano, kila upande ukituhumiana kukosa uwazi na uaminifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *