
Mwanamuziki Eddy Kenzo amemtabiria mema rapa Gravitty Omutujju kwa kusema kuwa atapata mafanikio makubwa kwenye muziki wake licha ya watu kumpiga vita kila mara kwenye shughuli zake.
Kwemye mahojiano yakw hivi karibuni Kenzo amesema omutujju hatoshushwa kisanaa na baadhi ya watu wanaojaribu kumshambulia mtandaoni kwani ni moja kati ya watu ambao wamepitia maisha ya taabu..
“Nilimtoa Gravity kutoka mitaa ya banda. Alikuwa analala chumba kimoja na mama yake mzazi pamoja na dada yake. Ana ujasiri kwa kile anachokifanya najua atafika mbali, hivyo hakuna mtu ambaye atamshusha kisanaa mapema, ana moyo mugumu wa kupigana na matatizo”, Alisema.
Eddy Kenzo ambaye alimtoa kimuziki Rapa Gravityy Omutujju chini ya lebo yake ya muziki ya Big Talent, anatarajiwa kufanya tamasha lake la muziki Novemba 9 mwaka huu huko Kololo Airstrip nchini Uganda.