Nyota wa muziki kutoka Uganda, Eddy Kenzo, ameweka historia kwa kuwa mwakilishi pekee wa Afrika Mashariki kwenye tuzo za Grammy mwaka 2026. Kenzo amechaguliwa kuwania kipengele cha Best African Music Performance kupitia wimbo wake “Hope & Love” aliomshirikisha mwanamuziki na mtayarishaji maarufu wa vyombo vya muziki, Mehran Martin.
Wimbo huo unamenyana na nyimbo kubwa kutoka kwa mastaa wa Afrika wakiwemo Burna Boy kupitia “Love”, Davido na Omah Lay kwa “With You”, Ayra Starr na Wizkid kupitia “Gimme Dat”, pamoja na Tyla kupitia “Push 2 Start”.
Tuzo hizo za Grammy 2026 zimeonekana kuwa na ushindani mkubwa zaidi katika kipengele hicho, zikionyesha jinsi muziki wa Afrika unavyozidi kupata kutambulika kimataifa.
Sherehe za utoaji wa tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Los Angeles, California, mwaka 2026, na Eddy Kenzo ameonyesha kuwa muziki wa Afrika Mashariki una nafasi kubwa kwenye jukwaa la kimataifa.