Msanii chipukizi kutoka Tanzania Pipi Jojo, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya video yake kusambaa ikimuonyesha akicheza kwa mitindo ya kimahaba mbele ya bosi wake Chief Godlove, ambaye alikuwa ameketi sebuleni akitazama runinga.
Katika video hiyo, Pipi Jojo alionekana akikata mauno kwa ustadi na hisia kali huku akimuangalia moja kwa moja Chief Godlove, jambo lililowafanya baadhi ya mashabiki kuanza kuhoji aina ya uhusiano uliopo kati yao.
Wengi wamehoji kama kweli ni uhusiano wa kazi pekee au kuna ukaribu zaidi, hasa ikizingatiwa kwamba msanii huyo amekuwa akimuita Chief Godlove “baba” kwenye mahojiano na machapisho yake ya mitandaoni.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wamemtetea Pipi Jojo wakisema video hiyo ilirekodiwa kama sehemu ya promo ya “Chakacha Challenge”, iliyoanzishwa na Chief Godlove kuhamasisha watu kucheza wimbo huo ambapo washindi wanatarajiwa kujinyakulia zawadi nono ikiwemo milioni 5 kwa mshindi wa kwanza.