Entertainment

Eddy Kenzo sio gwiji wa muziki – Bebe Cool

Eddy Kenzo sio gwiji wa muziki – Bebe Cool

Msanii Bebe Cool amedai kwamba Eddy Kenzo hana vigezo vya kuitwa lejendari kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Kwenye mahojiano hivi karibuni amesema hitmaker huyo wa “Nsimbudde” ana mengi ya kufanya kwenye muziki kama kweli anataka kufikia hadhi ya kuitwa nguli.

Bosi huyo wa Gagamel anasema Eddy Kenzo ni msanii mwenye bahati tu na anaweza kushinda tuzo ya Grammy mwaka 2023.

“Eddy Kenzo ni mwanamuziki mzuri lakini hajavuka mstari wa kuitwa nguli, hata kwa tuzo alizoshinda. Inabidi atie bidii zaidi ili kufikia viwango vya Chameleone, Bobi Wine, na mimi mwenyewe. Sio tu kwa nyimbo na tuzo,” alisema.

Utakumbuka juzi kati, Bebe Cool alitoa orodha yake ya kila mwaka ya wasanii waliofanya vizuri mwaka 2022.

Bebe Cool aliwataja wanamuziki anaoamini wamepata hadhi ya kuitwa malejendari kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda.

Kwenye orodha hiyo aliwataja; Jose Chameleone, Bobi Wine, Afrigo Band, na Maddox Sematimba huku akisisitiza kuwa wanaweza kukaa bila kutoa wimbo mkali kwa miaka mingi ijayo kutokana nyimbo zisizochuja walizoziachia miaka ya hapo nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *