Entertainment

Eddy Kenzo sio mwanamuziki bora Uganda – Ragga Dee

Eddy Kenzo sio mwanamuziki bora Uganda – Ragga Dee

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Ragga Dee amemkataa Bosi wa Big Talent, Eddy Kenzo.

Hii  ni  baada ya watu kuhoji kuwa Eddy Kenzo ndiye mwanamuziki bora nchini humo kufuatia kuteuliwa kwake kwenye tuzo za Grammy mwaka 2023.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Ragga Dee amesema kuna wasanii wengi nchini Uganda ambao wana vipaji kumzidi Kenzo, hivyo kwa upande wake haamini kama hitmaker huyo “Nsimbudde” hapaswi kupewa taji la mwanamuziki bora nchini humo.

“Eddy Kenzo ni msanii mzuri sana, hata hivyo, sio mwanamuziki bora nchini Uganda. Kuna wasanii wengine wazuri wa Karamoja na mikoa mbalimbali ambao hatuwajui,” alisema.

Ikumbukwe kipindi cha nyuma Kenzo alisema kwamba hajali maneno ya watu wanaodai kuwa yeye ni msanii bora nchini uganda, ila jambo analozingatia kwenye muziki wake ni kufanya kazi zenye ubora.

Wasanii kadhaa ikiwemo Gravity Omutujju na Roden Y Kabako wanamtaja Eddy Kenzo kama mwanamuziki bora nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *