
Mchekeshaji Eric Omondi amewatolea uvivu mameneja wa msanii Stevo Simple Boy kwa kushinda kumkingia kifua msanii huyo alipwe pesa zake kabla ya kutumbuiza kwenye tamasha la SolFire Fiesta.
Kupitia instastory yake mchekeshaji huyo ameandika ujumbe wa masikitiko kwenda kwa uongozi wa Stevo ambao kwa mujibu wake ulitumia kiasi cha shilling 84,000 kwa chakula huku wakimuacha msanii huyo akiwa hajalipwa chochote.
Aidha ametaka uongozi wa Men In Business kujiuzulu mara moja la sivyo atahakikisha wanafungulia mashataka ya utapeli huku akihoji ni kwa nini Stevo Simple Boy anasimamiwa na mameneja wanne tofauti na wasanii wengine.
Kauli ya Omondi imekuja siku moja baada ya stevo na uongozi wake kutoa taarifa kwa umma wakieleza ghadhabu zao kwa waandaji wa SolFire Fiesta kwa kushindwa kutoa malipo yote kabla ya Stevo kupanda jukwaani.