Entertainment

Eric Omondi Asema Vijana Ndio Nguzo ya Kutimiza Ndoto ya Raila

Eric Omondi Asema Vijana Ndio Nguzo ya Kutimiza Ndoto ya Raila

Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, Eric Omondi, ametoa wito kwa vijana wa taifa hilo kusimama pamoja kwa umoja na kuendeleza urithi wa hayati Raila Odinga kwa vitendo.

Kupitia ujumbe wake kwa vijana, Eric amesema kuwa wakati taifa la Kenya linaendelea kuomboleza kifo cha kiongozi huyo, ni jukumu la vijana kutimiza yale yote ambayo Raila alianza lakini hayakukamilika enzi za uhai wake..

Mchekeshaji huyo aliyegeukia uanaharakati, amesema vijana wa Kenya wana fursa kubwa kumaliza kazi hiyo, kwani wao ndio nguvu kuu ya taifa na walikuwa sehemu muhimu ya maono ya Raila kuhusu haki, umoja na maendeleo.

Kauli ya Omondi inakuja wakati amekuwa akiendeleza kampeni za kuwarai vijana wa Gen Z kujisajili kama wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, akisisitiza kuwa ni kupitia kura pekee ndipo vijana wataweza kutimiza maono na ndoto ya Kenya mpya yenye usawa, matumaini na haki kwa wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *